• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watafiti waanza majaribio ya chanjo ya Ebola nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2014-12-19 17:25:03

    Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya imeanza kuifanyia majaribio kwa binaadamu chanjo iliyotengenezwa kwa ajili ya kuzuia virusi vya Ebola.

    Taarifa kutoka taasisi hiyo imesema wataalamu wa mpango wa utafiti wa Wellcome Trust katika mji wa Kilifi wametoa dozi ya kwanza ya chanjo ya VSV-Ebola kwa wahudumu wa afya katika hospitali za huko. Mkurugenzi wa taasisi hiyo profesa Solomon Mpoke amesema majaribio hayo ambayo yanatarajiwa kuweza kupatikana kwa haraka matibabu yenye ufanisi dhidi ya ugonjwa, yanalenga wahudumu wa afya kutokana na kuwashughulikia wagonjwa wa Ebola.

    Amesema majaribio haya, na mengine yanayofanyika nchini Marekani, Ujerumani, Uswisi na Gabon, yatajaribu usalama wa chanjo na uwezo wake wa kuzalisha mfumo wa kinga kwa watu wazima wenye afya nzuri.

    Habari nyingine zinasema waziri wa afya wa Guinea Bissau Valentina Mendes amesema China iko kwenye mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za nchi dhidi ya Ebola. Amesema mwezi Aprili mwaka huu, China ilikuwa ya kwanza kutuma vifaa vya matibabu vyenye thamani ya dola kimarekani laki 2 kwa Guinea Bissau ili kuzuia ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako