• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatuma kundi la pili la wataalam wa afya kusaidia kupambana na Ebola Siera Leone

    (GMT+08:00) 2014-12-20 20:24:39

    Kundi la pili la wataalam wa afya wachina limeondoka leo mjini Beijing kwenda Siera Leone kusaidia juhudi za kukinga na kudhibiti maambukizi ya Ebola nchini humo.

    Kundi hilo lenye wataalam 14 wa kuzuia na kudhibiti magonjwa ya maambukizi, magonjwa ya mlipuko, elimu ya afya na vipimo vya maabara, linatarajiwa kutoa mafunzo kwa watu maofisa elfu 4 nchini Sierla Leone.

    Vifaa vya tani 2.4 vinavyojumuisha vitabu vya mafunzo na video, vifaa vya kujikinga, upimaji wa joto pamoja na dawa pia zimesafirishwa nchini Siera Leone.

    Kundi la kwanza la wataalam 12 wa kupambana na Ebola lilikwenda Siera Leone Novemba 19 ambako limefanikiwa kutoa mafunzo kwa watu elfu 2 jinsi ya kudhibiti na kuzuia kuenea kwa Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako