• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kuimarisha hatua za kuzuia Ebola Afrika Magharibi

    (GMT+08:00) 2014-12-22 10:46:23

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema ingawa ugonjwa wa Ebola nchini Mali umedhibitiwa, virusi ya Ebola bado ni tishio, nchi za Afrika ya Magharibi zinatakiwa kufuatilia na kuimarisha hatua za kuzuia ugonjwa huo katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

    Bw Ban Ki Moon pia amekutana Rais Keita wa Mali na kusifu hatua zilizochukuliwa na serikali ya Mali katika kukabiliana na Ebola. Pia wamezungumzia masuala kuhusu mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Mali na kundi la wanamgambo wa kaskazini mwa nchi hiyo. Bw. Ban pia ametoa wito kwa serikali ya Mali kushiriki katika mazungumzo ya amani, na kusema usalama na utulivu ni njia ya pekee ya kutimiza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako