• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bondia Anthony Crolla aapa kurejea akiwa na nguvu zaidi, Khan kwenda Pakistan

    (GMT+08:00) 2014-12-22 15:28:55

    Bondia Anthony Crolla ameapa kurejea akiwa na nguvu zaidi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya fuvu la kichwa na kuvunjika mguu alipojaribu kupambana na wezi. Crolla amelazimika kujitoa kwenye pambano lake la kuwania mkanda wa lightweight na Mcuba Richar Abril lililopangwa kufanyika Januari. Bondia huyo aliwaona wezi wawili wakikimbia nyuma ya bustani ya nyumba ya jirani huko Chadderton, Greater Manchester, na kupigwa kwa kitu kizito kwenye tukio hilo. Wakati huohuo bondia wa uingereza Amir Khan anatarajiwa kwenda Pakistan, mwishoni mwa mwezi huu ili kuonyesha ushirikano kwa waathirika wa mauaji ya shule ya kijeshi ya Peshawar. Wanamgambo wa Taliban waliwaua watu 141 katika tukio hilo. Wazazi wa bondia huyo walizaliwa nchi Pakistan, Khan atachangia kaptula za kupigania ndondi zenye thamani ya pauni elfu 30 kwa ajili ya ujenzi mpya wa shule. Khan amesema anachofanya ni kuwaambia watu kuwa kinachotendeka ni makosa. Khan mwenye miaka 28 anatarajia kusafiri kwenda Pakistan kati ya krisimas na mwaka mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako