• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid wawa mabingwa wapya wa klabu bingwa duniani

    (GMT+08:00) 2014-12-22 15:30:23

    Klabu ya Real Madrid ya Hispania juzi ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa klabu bingwa duniani wakiwarithi FC Bayern Munich. Wakicheza kwenye uwanja wa Marrekech, nchini Morocco Madrid walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya San Lorenzo na kufanya idadi ya makombe waliyochukua kufikia matatu kwani walianza na Copa Del Rey, kisha Champion League na sasa klabu bingwa duniani. Sergio Ramos na Gareth Bale walifunga magoli ya ushindi katika mchezo huo. Kwa ushindi huo Real Madrid wameweka rikodi ya kuchukua ubingwa huu wa dunia kwa vilabu kwa mara ya kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako