• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo azindua sanamu yake ya kuenzi mafanikio yake

    (GMT+08:00) 2014-12-22 15:31:01

    Cristiano Ronaldo amezindua sanamu yake ya kuenzi mafanikio yake, katika mji aliozaliwa wa Funchal kwenye Kisiwa cha Madeira. Akizungumza katika uzinduzi huo maalumu huku akizungukwa na Familia yake pamoja na Maelfu ya Mashabiki, Ronaldo alieleza kwamba huo ulikuwa ni wakati maalumu kwake, kuweka Sanamu yake. Dolores Aveiro mama yake Ronaldo aliongeza kwa kusema Ronaldo hajawahi kusahau asili yake. Sanamu hiyo yenye Urefu wa Mita 3.4 ni sehemu ya mkusanyiko wa Mataji na Tuzo mbalimbali ambazo amezitwaa katika maisha yake ya Soka na kuhifadhiwa kwenye Makumbusho yake maalum hapo Kisiwani Madeira zikiwemo tuzo za Ballon d'Or. Ronaldo amefunga jumla ya magoli 34 katika michezo 27 msimu huu, na anawania tuzo ya mchezaji bora wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako