Hali ya bondia mashuhuri Muhammad Ali imeimarika vizuri tangu apelekwe hospitali kutokana na ugonjwa wa nimonia. Bob Gunnell amesema daktari wa Ali anategemea kumruhusu hivi karibuni. Pia amesema familia ya Ali inaomba ipatiwe faragha na kushukuru kwa maombi yote ya kumtakia Ali apone na awe na afya njema. Bondia huyo wa zamani mwenye miaka 72 ambaye ni bingwa mara tatu wa uzito wa juu, mwenye ugonjwa wa Parkinson, alipelekwa hospitali siku ya Jumamosi. Bwana Gunnel hakutoa taarifa zaidi. Ali aligundulika kuwa na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kustaafu ndondi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |