• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Van Gaal adai kushindwa kuzifunga timu ndogo kutawakosesha ubingwa

    (GMT+08:00) 2014-12-23 14:15:45

    kocha Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal, anaamini kwamba kikosi chake kinaweza kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, lakini hilo haliwezi kutokea kwa kushindwa kuzifunga timu ndogo. Mdachi huyo alikerwa na matokeo ya sare ya bao 1-1 iliyovuna timu yake dhidi ya Aston Villa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika juzi Jumamosi. Kwenye mchezo huo uliofanyika Villa Park, Man United iliduwazwa kwa bao la mapema kutoka kwa straika Christian Benteke kabla ya kusawazisha kipindi cha pili kupitia mshambuliaji Radamel Falcao. Kitu kilichomkera zaidi Van Gaal ni kwamba sare hiyo iliyopata timu yake ni dhidi ya Aston Villa iliyokuwa pungufu uwanjani kwa zaidi ya dakika 25, hivyo walishindwa kutumia vizuri nafasi hiyo kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa ligi hiyo Chelsea. Kwa sasa pengo ni pointi kumi, wakati Chelsea jana Jumatatu ilicheza na Stoke City uwanjani Britannia na kuwachabanga mabao 2-0 na kuendelea kujihakikishia kuwa bado wataendelea kuwa vinara wa ligi ya Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako