• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chanjo ya Ebola inayofanyiwa majaribio nchini Uganda ni salama

    (GMT+08:00) 2014-12-24 20:27:25

    Wanasayansi kutoka Marekani wamesema aina mbili za chanjo za Ebola zinazofanyiwa majaribio ni salama, na zimetoa kinga inayofanana kwa Waganda wenye afya nzuri.

    Katika majaribio ya awamu ya kwanza, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda waliwafanyia majaribio watu 108 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 50. Matokeo ya majaribio hayo yalionyesha kuwa, watu hao hawakupata madhara yoyote kutokana na chanjo hiyo.

    Mwanasayansi kutoka idara ya kitaifa ya Marekani ya utafiti wa afya anayeongoza mradi huo Julie Ledgerwood amesema, habari hii inatia moyo, kwa kuwa imeweka msingi wa upatikanaji wa chanjo yenye ufanisi zaidi.

    Wakati huohuo, kituo cha matibabu ya Ebola kilichofadhiliwa na China nchini Liberia jana kilimpokea mgonjwa wa kwanza wa Ebola.

    Mkuu wa kikosi cha madakrati cha China nchini humo Wang Yungui amesema, mgonjwa huyo alipelekwa katika kituo hicho jumatatu mchana, na alikuwa na homa, kuharisha na kutapika. Baada ya kupimwa, mgonjwa huyo alithibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola.

    Tangu kituo hicho kifunguliwe Desemba 5, kimewapokea wagonjwa 37 na kulaza wagonjwa 27 wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako