• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa China wataka kuwepo kwa mtandao wa uhakikisho wa jamii wenye haki na ufanisi

    (GMT+08:00) 2014-12-25 10:03:11

    Wabunge wa China wametaka kuwepo kwa mfumo wa uhakikisho wa jamii wenye ufanisi na umoja.

    Kwenye mkutano wa kujadili ripoti ya baraza la serikali ya China kuhusu uhakikisho wa jamii, wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la China wameitaka serikali kuhamasisha kuunganisha programu zote za uhakikisho wa jamii.

    Kwa sasa China ina programu tofauti za uhakikisho wa jamii kwa wakazi wa vijijini, wakazi wa mijini wasioajiriwa, na wakazi wa mijini walioajiriwa.

    Mbali na hayo kuna pengo kubwa kati ya programu za uhakikisho wa jamii kati ya miji ya mashariki mwa China iliyopiga hatua kiuchumi, na miji ya magharibi. Wajumbe wa kamati hiyo pia wametoa mwito kuwa utaratibu wa uhakikisho wa jamii usitofautishe watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako