• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wada yachukua sampuli 3,000 za damu kutoka kwa wanariadha wa Russia

    (GMT+08:00) 2014-12-25 14:04:28

    Karibu sampuli 3,000 za wanariadha zimechukuliwa na maofisa wa Russia wanaochnguza madai ya kuenea matumizi ya dawa za kuongeza nguvu nchi humo. Shirika la kupambana na dawa za kuongeza nguvu WADA limeanzisha uchunguzi wake kufuatia madai yaliyotolewa kwenye dokumentari iliyorushwa na televisheni ya Ujerumani. Waziri wa michezo wa Russia Vitaly Mutko amesema kuwa tume ya Wada sasa imetembela nchini humo kuchunguza madai na kuchukua sampuli hizo ili kuchunguzwa kwenye maabara. Mutko amefafanua kuwa ameandika barua kwa Wada na kuwaambia kuwa Russia iko wazi kupokea tume yoyote ya uchunguzi na wapo tayari kuonesha kila kitu. Ilidaiwa kuwa orodha ya saampuli za damu za wanariadha 150 zinazohisiwa, zikiwemo ya mmoja kutoka Uingereza, hazikuchunguzwa kwa makini na shirikisho la wanariadha la kimataifa. Mapema mwezi huu Wada ilimtangaza mkuu wake wa zamani Dick Pound kuongoza tume ya uchunguzi na kuangalia madai ya Ujerumani, lakini imesema haitaanza kazi hadi Januari 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako