• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maabara ya China yashiriki kwenye operesheni ya kinga na udhibiti wa Ebola Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2014-12-26 10:39:44

    Wiki moja iliyopita mji wa Freetown ulianzisha operesheni ya mwezi mmoja ya kinga na udhibiti wa Ebola, na upimaji haraka wa virusi katika maabara ya China kwenye hospitali ya urafiki kati ya China na Sierra Leone ni sehemu muhimu ya operesheni hiyo. Imefahamika kuwa, wafanyakazi wa upimaji wa China wameitikia operesheni hiyo na kurekebisha kwa wakati mpango wa upimaji, ili kuhakikisha matokeo ya upimaji yanatolewa ndani ya siku moja.

    Wataalam wa Shirika la Afya Duniani WHO hivi karibuni wamefanya ukaguzi kwenye kituo cha uangalizi cha Ebola cha China nchini Sierra Leone, na kuona kuwa kituo hicho kina miundombinu kamili, na kinafanya kazi kwa kufuata kwa makini vigezo husika vya WHO.

    Sierra Leone imetangaza karantini ya siku tano katika sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo kuanzia mkesha wa Krismasi. Mkuu wa sehemu hiyo Alieu Kamara amesema karantini hiyo ina lengo la kuimarisha udhibiti kwa virusi vya Ebola na kuzuia visienee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako