nyumbani
|
Hivi karibuni matukio ya yaya kuwatesa watoto yalionyeshwa kwenye runinga za Afrika mashariki. Matukio hayo mbali na kuzua hisia tofauti miongoni mwa jamii yaliwafanya wazazi haswa kina mama kufikiria upya ni nani wa kuajiri kama yaya.
Hata hivyo kulingana na washauari wa maswala ya kifamilia uhusiano mbaya kati ya yaya na mwajiri wake ni njia moja inayoweza kupelekea vitendo kama hivyo vya kuwatesa watoto.
Ronald Mutie anaripoti.
Beatrice Mwanzia ni mfanyikazi wa nyumba mjini Nairobi Kenya.
Yeye kama wakaazi wengi aliona kwenye runinga tukio la yaya akitesa mtoto wa mwajiri wake. Anasema licha ya kwamba wakati mwingine watoto huwa watundu anayewalea anafaa kuwa na kipimo cha adhabu.
"siwezi kufanya hivyo hata hawa watoto wakinikosea nanyamza na baadaye naambia mama yao. Lakini wakati naona amefanya kosa na kweli nahitaji kumchapa nitafanya hivyo lakini siwezi kumchapa aumie ni kumtoa ile makosa amefanya kwa sababu nikiwachana naye ataaribika"
Matukio mawili ya yaya wakitesa watoto yalinaswa kwenye kamera iliowekwa nyumbani.
Hiyo ina maana kwamba kuna matukio mengine kama hayo yanafanyika lakini kwa sababu hakuna kamera kwenye nyumba nyingi za makaazi yaya wanaofanya hivyo hawawezi kujulikana huku nao watoto wanaodhulimiwa wakikosa kuripoti kwa sababu ya umri wao mdogo.
Hii imewafanya wazazi wengi kama vile Lydiah Kwamboka kuanza kutumia teknolojia ili kuhakikisha usalama wa watoto wao wanapokuwa nje ya nyumba.
"nikiwa na uwezo nitaweka kamera kwa nyumba yangu. Kwa sababu kama umeweka kamera ukiwa kazini hautakuwa na wasiwasi . Pia naona ni vizuri ukiajiri msichana wa kazi kwanza akupee kitambulisho chake na uchunguze kwenye ametokakwa sababu unapomajiri uamwachia kila kitu kwa nyumba na ndio anabeba maisha yenu na uspomchunguza labda anayweza kuwafanyia kitu nyinyi wote."
Lakini mshauri wa mambo ya jamiii Bi Anne Nafula anaona kwamba kuweka mitambo ya kamera sio suluhu la kutosha kwa maswala kama haya.
"Lazima mwajiri aelewe kwamba mfanyikazi nyumbani sio mfanbyikazi tu anafaa amuweke kama mmoja wa uko ama jamii ili akuangalilie mtoto kwa njia zuri lakini ukimchukulia kwamba huna muda na nyumba yako basi atafanya vile anavyopenda"
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari ni wazi matukio ya yaya kuolewa na ama kupata watoto na waajiri wao yameongezeka.
Bi Nafula analaumu baadhi ya wanawake walioolewa kwa kutelekeza majukumu yao ya kumwaachia yaya kufanya shughuli zote za nyumba.
"yale majukumu yangefanywa na mke wa nyumba yanapatiwa msichana wa kazi wanawake wameshindwa na majukumu yao hata ya kulea watoto, hata kuangalia mabwana zao. Na wanaume hawaangali sana urembo inapofika kwa swala la mapenzi, wanaangalia Yule anayemletea chakula, kumpelekea maji ya kuoga, maji ya kunywa. kwa mfano kuna watu wawili mawakili waliofunga ndoa lakini mke alikuwa hashughuliki siku zote alikaa tu kusoma gazeti na kutengeneza kucha. Hatimaye huyo mwanamme alioa huyo yaya na wakazaa watoto wawili na akamnunulia nyumba"
Kulingana na sheria za Uganda kitendo cha kumfanyia mtoto mateso kinahadhibiwa kwa kufungwa hadi miaka 15 gerezani na nchini Kenya adhabu ya kosa hilo ni zaidi ya miaka kumi.
Lakini kulingana na Nafula ni vyema mama wa nyumba kujenbga urafiki na mwajiri wake kutapunguza kwa asilimia kubwa sio tu kuteswa kwa watoto mbali pia na kuwa na familia imara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |