• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shindano la Miss Tanzania lasitishwa kwa muda wa misimu miwili

    (GMT+08:00) 2014-12-26 14:18:56
    Shindano la Miss Tanzania limesimamishwa kwa muda wa misimu miwili ili kutoa fursa kwa waandaaji wa shindano hilo kurekebisha baadhi ya kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa mara kwa mara. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza amesema serikali kupitia baraza hilo imefikia umamuzi huo kutokana na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wadau mbalimbali na wapenzi wa shindano hilo. Amesema imefika wakati sasa waandaji warekebishe masuala kadha ili kuondoa malalamiko na manung'uniko miongoni mwa wadau ili kulipa heshima shindano hilo, pia liweze kuheshimika na kila mtu.
    Mngereza ameongeza kuwa, serikali kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imelipa dhamana baraza hilo kisheria kushughulikia masuala yote yanahusu sanaa na Utamaduni hivyo baraza lina mamlaka ya kuingilia kati endapo litajiridhisha kuwa kuna masuala hayaendi sawasawa. Kuhusiana na sakata la umri wa aliyeshinda shindano hilo kwa mwaka 2014 Sitti Mtemvu, Mngereza amesema suala la kuthibitisha umri wa mrembo huyo linafanyiwa kazi na Mamlaka husika ambayo ni RITA, na kwamba BASATA haihusiki nalo kabisa. Amemalizia kwa kusema kuwa mrembo Lilian Kamazima aliyetwaa taji hilo baada ya kuvuliwa na Sitti Mtemvu ataendelea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia kwa mwaka 2015 kama ilivyopangwa, lakini hakutakuwa na mashindano mengine kwa kipindi cha miaka miwili ndani ya Tanzania kuanzia ngazi ya vitongoji.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako