Mbio za Man United kuchukua taji zagonga mwamba
(GMT+08:00) 2014-12-29 14:00:01
Mbio za Manchester United kujaribu kuwafikia Chelsea na mabingwa wa ligi hiyo Manchester City ziligonga mwamba baada ya kuambula sare ya 0-0 walipocheza na Totenham Hotspurs. United ilipata nafasi nyingi nzuri katika kipindi cha kwanza huku shambulizi la Juan Mata likipiga mwamba wa goli. Hata hivyo mlinda mlango wa Totenham Hugo Lloris alilazimika kufanya kazi ya ziada kuzuia mabao ya Radamel Falcao, Robin Van Persie na Ashley Young. Naye kiungo wa kati wa Spurs Andros Townsend alifanya mashambulizi makali katika ngome ya manchester United huku Ryan Mason akikosa bao la wazi katika dakika za mwisho. Kikosi hicho cha Mauriccio Pochettino kimekuwa kikifunga mabao yake katika dakika za lala salama dhidi ya Swansea na Leicester lakini licha ya kudhibiti mpira dakika 15 za mwisho katika kipindi cha pili hawakuweza kupata bao.