Usajili wa Fernando Torres waiva klabuni Atletico Madrid
(GMT+08:00) 2014-12-29 14:00:28
Siku za Fernando Torres kutajwa kama mshambuliaji wa Ac Milan na Chelsea zinazidi kukaribia kufikia mwisho baada ya usajili wa mchezaji huyo ndani ya timu yake ya zamani ya Atletico Madrid kukamilika. Tayari makubaliano baina ya pande zote zinazohusika yamefikiwa na kilichobaki na kwa mikataba rasmi kutiwa saini na inatarajiwa kuwa mpaka kufikia tarehe 30 ya mwezi huu yaani kesho Torres ataanza kufanya mazoezi na kikosi cha Diego Simeone. Habari toka huko nchini Hispania zinasema kuwa wawakilishi wa pande zote zinazohusika kwenye makubaliano haya walikutana siku ya jumamosi na kufanya mazungumzo ambayo yaliashiria makubaliano ya msingi juu ya usajili wa wachezaji hawa wawili Torres na Cerci. Hii itakuwa mara ya pili kwa Fernando Torres kufanya kazi na Diego Simeone baada ya wawili hawa kuwa pamoja kama wachezaji katika miaka ya 2000 wakati Torres alipokuwa anaanza maisha yake kama mshambuliaji chipukizi kwenye kikosi cha Atletico Madrid.