• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 2014 watajwa kuwa mwaka mbaya zaidi kwa makocha wa Kenya

    (GMT+08:00) 2014-12-30 14:25:07
    Wachambuzi wa soka nchini Kenya wameutaja mwaka wa 2014 kuwa mbaya zaidi kwa makocha wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu nchini humo. Ni mwaka ambao umeshuhudia makocha wengi wakitimuliwa akiwemo James Nandwa na naibu wake Mickey T9" Weche licha ya kuiwezesha klabu ya FC leopard kutwaa ngao ya GOTV mwaka wa 2013. Licha ya kuunda uhusiano mzuri na wachezaji wake, Nandwa alitimuliwa vibaya mwaka huu kutokana na matokeo ya mabaya ya klabu hiyo. Juma Abdalla wa Kenya Commercial Bank ni kocha mwengine ambaye aliangukiwa na shoka la kutimuliwa mwaka huu licha ya kuandikisha matokeo mazuri kwa klabu hiyo 2013. Wengine ni kocha wa Ujerumani aliyekuwa akiifunza Nakuru All Stars ambaye alitimuliwa baada ya mechi 3 tu za klabu hiyo. Mwengine aliyejiondoa kwenye klabu kutokana na matatizo ya kifedha ni kocha Mnigeria wa City Stars Robinson Ofwoku. Wadadisi wa mambo ya soka wanaona hali hiyo huenda itashuhudiwa tena katika msimu mpya wa mwaka mpya wa 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako