• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti waonesha kuwa popo ni chanzo cha ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi

    (GMT+08:00) 2014-12-31 10:00:04

    Utafiti uliofanya na taasisi ya Robert Koch ya Berlin Ujerumani unaonesha kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa Ebola unaoenea katika nchi za Afrika Magharibi ulitoka kwa popo.

    Utafiti wa wiki nne uliofanyika nchini Guinea mwezi April kuangalia hatari inayoweza kuwakuta binadamu baada ya kukaribiana na popo, na kuchukua sampuli ya popo kutoka eneo la Meliandou la Guinea na misitu ya karibu. Virusi vilivyoenea kutoka Meliandou ndio vilienea katika maeneo mengine ya Guinea, na nchini sierra Leone, Liberia, Nigeria na Senegal.

    Habari nyingine zinasema Benki Kuu ya Liberia imetangaza hatua za kupunguza madhara kwa uchumi kutokana na ugonjwa wa Ebola, kwenye mfumo wa benki na kwenye uchumi kwa ujumla. Hatua hizo ni pamoja na kuzisaidia shule zilizofungwa kutokana na karantini ya Ebola, kulipa madeni yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako