Nahodha wa timu ya soka ya Uholanzi na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo Januari 13 huko Zurich nchini Uswisi alishinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya pili, na kumaliza utawala wa Lionel Messi wa Argentina ambaye alishinda mara nne. Wakati huohuo Ronaldo ameweka rikodi mpya katika msimu mmoja wa mwaka 2013/14 kwa kuwa kinara wa kufunga magoli mengi katika ligi ya mabingwa kwa kufunga magoli 17 na kuisaidia Real Madrid kushinda taji la ligi ya mabingwa. Naye Lionel Messi amevunja rikodi mbili na kuwa mfungaji bora katika historia ya ligi ya Hispania La Liga na ligi ya mabingwa akiwa na miaka 27 huku akiwa amefunga magoli 253 katika mechi 189 alizocheza na kuipiku rikodi ya Telmo Zarra ya miaka 59 kwenye La Liga, pia amefunga magoli 74 katika ligi ya mabingwa na kumpita mchezaji mashuhuri wa Real Madrid Raul.
NBA ilifanya mabadiliko mawili muhimu mwaka 2014, moja ni David Stern ambaye alijiuliza nafasi yake ya kamishna wa NBA Februari 1 baada ya miaka 30 ya uongozi. Stern alianza kuongoza Februari 1 maka 1984. nafasi yake imechukuliwa na Adama Silver. Mwengine ni Donald Sterling aliyekuwa mmiliki wa Clippes amejiuzulu baada ya timu hiyo kuuziwa mkurugenzi wa zamani wa Microsoft Steve Ballmer kwa bilioni 2 za Kimarekani Agosti 12. Sterlin alipigwa marufuku ya maisha na NBA kufuatia kashfa ya kutoa kauli za ubaguzi wa rangi.
Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ilifanyika huko Sochi nchini Rusia kuanzia Februari 7 hadi 23. Nchi na sehemu 88 zilishiriki kwenye michezo hiyo ya Sochi ambayo imeshirikisha vitengo 98. katika michezo hiyo rikodi 10 ziliwekwa.
Tukio lingine kubwa litakalokumbuka mwaka huu ni michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazil ambayo ilianzia Juni 12 hadi Julai 13. Wenyeji Brazil walitia aibu kwa kuchapwa mabao 7-1 na Ujerumani kwenye nusu fainali na kufanikiwa kuingia hatua ya fainali ambapo walichuana na Argentina na hatimaye Ujerumani kuibuka washindi wa kombe hilo baada ya kushinda kwa bao 1-0. Mabingwa watetezi Hispania walishindwa kutamba na kufika hatua 16 bora. James Rodriguez kutoka Colombia alishinda kiatu cha dhahabu. Mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose amepora nafasi ya mchezaji mashuhuri Ronaldo na kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kwenye kombe la dunia.
Naye Novak Djokovic ametajwa kuwa namba moja duniani kwa mara ya tatu pia amepata mataji kwenye michuano ya Wimbledon na michuano ya Masters.
Wakati huohuo mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius naye aliingia kwenye vitabu vya historia mwaka 2014 baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano kufuatia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Mwanariadha huyo wa kimataifa hataruhusiwa kushiriki mashindano yoyote ya riadha kwa miaka mitano atakayokuwa jela hata ikiwa ataachiliwa kabla ya miaka hiyo kukamilika.
Fifa imetoa taarifa ya kuzisafisha Russia na Qatar kuhusu kashfa za rushwa inazozikabili nchi hizo wakati wa kinyang'anyiro cha kuwania kuwa nchi mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na 2022. Hata hivyo rais wa Fifa Sep Blatter alikataa kutoa ripoti kamili ya uchunguzi, ambayo ilizua maswali mengi akiwemo rais wa Uefa Michael Platini na wakili aliyeendesha uchunguzi huo Michael Garcia, akaamua kujiuzulu.
dokumentari iliyotolewa na televisheni moja nchini Ujerumani ARD mwezi Disemba ilisababisha utata mkubwa ambapo iliituhumu Russia kwa kuruhusu wanariadha wake kutumia dawa za kuongeza nguvu na kuwafichia michezoni. Miongoni mwa waliotajwa kuhusika ni pamoja na Maria Savinova na mshindi wa mara tatu wa Marathoni ya Chicago Liliya Shobukhova..
Muingereza Lewis Hamilton mwaka huu alitamba kwenye mashindano ya mbio za magari ya Russia Grand Prix na kuchukua ushindi kwa mara ya tisa, huku huu ukiwa wa nne mfululizo na kuendelea kutanua mbawa zake za ushindi. Pia alishinda katika mashindano ya langa langa ya US Grand prix.
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake. Naye Nahodha na mlinda mlango wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Senzo Meyiwa aliuawa baada ya kupigwa risasi. Tukio hilo liliripotiwa kutokea nyumbani kwa mpenzi wake Meyiwa huko Voloorus kusini mwa Johannesburg. Mbali na hayo mchezaji mmoja wa soka raia wa Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kichwani mwake kilichorushwa na mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria. Mechi hiyo ilikuwa ni kati ya JS Kabylie dhidi ya USM Alger.
Na habari ya mwisho ni kuhusu mechi ya kufuzu kombe la Ulaya kati ya Croatia na Italia ambayo ilisimamishwa baada ya mashabiki kurusha vitu vinavyowaka "flaire" uwanjani na kusababisha vurugu kiwanjani hapo. Mechi hiyo ya kundi H ambayo iliiisha kwa matokeo ya mabao 1-1, ilisimamishwa katika vipindi vyote viwili, huku wachezaji wakitolewa nje kwa dakika 10 na refa Bjorn Kuipers.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |