• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gunners kumnyemelea William Carvalho

    (GMT+08:00) 2015-01-01 11:09:39
    Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon William Carvalho mekuwa akilengwa na Gunners kwa mda mrefu licha ya kuwa na bei ghali. Klabu ya Sporting Lisbon inataka kitita cha pauni millioni 30, lakini kulingana na gazeti la daily mail nchini Uingereza kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kulipa pauni milioni 25.5. Vilevile Wenger ameripotiwa kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Newcastle Moussa Sissoko kwa kitita cha pauni millioni 9. Wakati huohuo meneja wa Manchester City Manuel Pelegrini anatarajiwa kumununua mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bonny ili kuchukua mahala pake Sergio Aguero ambaye ana jereha la mguu. Gazeti la Daily Telegraph limeripoti kuwa Manchester City pia inajiandaa kumnunua mshambuliaji huyo kwa takriban pauni millioni 30. Hatahivyo kulingana na The Times, Chelsea pia inamtaka mshambuliaji huyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako