• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maambukizi ya Ebola eneo la Afrika magharibi yanakaribia kudhibitiwa

    (GMT+08:00) 2015-01-01 18:35:22

    Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema, Guinea, Liberia na Sierra Leone zinakaribia kutimiza lengo la kufanya mazishi salama, kutenga na kutibu watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Ebola.

    Ripoti hiyo imesema, suala la kutokuwa na idadi kamili ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo na ukosefu wa vitanda vya kuwalaza wagonjwa bado ni changamoto kubwa kwa nchi hizo tatu.

    Hadi kufikia tarehe 28 mwezi uliopita, kesi za maambukizi ya Ebola katika nchi hizo tatu zimefikia 20,171, miongoni mwao, zaidi ya watu elfu 7 wamefariki dunia. Katika wiki tatu zilizopita, kesi mpya 1,416 za ugonjwa huo zimeripotiwa, miongoni mwao Sierra Leone inaongoza kwa kuwa na kesi 979.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako