• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya maambukizi ya Ebola yaelekea kutulia

    (GMT+08:00) 2015-01-02 09:52:29

    Takwimu kuhusu hali ya maambukizi ya Ebola zilizotolewa na Shirika la afya duniani WHO mwishoni mwa mwaka jana zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, watu 20,206 waliambukizwa Ebola, 7,905 kati yao walifariki kutokana na ugonjwa huo. Wakati mwaka mpya ulipowadia, nchi husika hazikulegeza tahadhari ili kuepusha ugonjwa huo usienee wakati wa sikukuu.

    Katika mwezi uliopita, idadi ya wagonjwa wapya walioambukizwa virusi vya Ebola ilipungua, lakini nchi za Afrika magharibi zilizoathiriwa vibaya na virusi hivyo bado zinachukua tahadhari, ili ugonjwa huo usizidi kuenea. Liberia ilitangaza kupiga marufuku kutoka nje katika mkesha wa mwaka mpya, ili kuepusha watu kuambukizwa virusi hivyo wanaposhiriki kwenye shughuli za umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako