• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yatangaza hakuna mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini humo

    (GMT+08:00) 2015-01-04 19:41:32

    Serikali ya Somalia leo imethibitisha kuwa hakuna mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini humo.

    Waziri wa afya wa Somalia Bw. Ali Mohamed Mohamud amekanusha habari zilizotolewa na vyombo vya habari vya Somalia kuhusu kesi ya mtu anayeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola katika mji wa Buulo Sharey, mkoani Shabelle.

    Bw. Mohamud amesema walichukua hatua za haraka na kumtenga mtu huyo baada ya kusikia uvumi huo.

    Bw. Mohamud amesema kuwa imebainika kuwa mtu huyo hana virusi hivyo lakini amepelekwa Mogadishu kufanyiwa vipimo zaidi na madaktari wa serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako