Klabu ya jijini London ya Arsenal itatangaza kumsajili kiungo wa Real Madrid Sami Khedira baada ya kufikia makubaliano na wawakilishi wa mchezaji huyo pamoja na viongozi wa Real Madrid. Kwa mujibu wa taarifa toka Hispania na England Arsenal imekubali kulipa paundi milioni 11 kwa ajili ya kiungo huyu mwenye asili ya Tunisia ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia nchini Brazil mwaka jana. Wakati huohuo Arsenal imemruhusu mshambuliaji wake Lukas Podolski kujiunga na mabingwa wa zamani wa ulaya Inter Milan zikiwa zimepita siku chache tangu kocha Arsene Wenger akanushe taarifa za mshambuliaji huyo kuondoka. Kwa upande wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City siku chache tu baada ya kuhusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji raia wa Ivory Coast Wilfred Bony, wametajwa kuongoza mbio za kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley na klabu hiyo imeandaa ofa ambayo ina uhakika kuwa haitakumbana na kikwazo chochote toka Everton na kwa mchezaji mwenyewe. Manchester City wanadaiwa kuwa wameandaaa ofa ya paundi milioni 45 kwa ajili ya mchezaji huyo huku wakiwa tayari kumvutia kwa dau nono la mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki kiasi ambacho kitakuwa kinauzidi mara mbili mshahara wake wa sasa. Hata hivyo Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha na kuwa mbioni kuihama klabu yake, Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling anatarajiwa kutia saini mkataba mpya utakaomfanya aingizie mshahara wa paundi 100,000 kwa mwezi akiwa amepandishiwa mshahara kutoka paundi 60,000 hivyo kuendelea kubaki na klabu hiyo kwa miaka mitano zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |