• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid yaula kwao mwaka wauanza kwa machungu

    (GMT+08:00) 2015-01-05 14:02:34

    Mabingwa wa Ulaya Real Madrid jana waliuanza vibaya mwaka 2015 baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Valencia katika mchezo wao wa 17 wa ligi kuu ya Hispania uliosakatwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Valencia Estadio Mestalla. Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Real Madrid tangu kuanza kwa mwaka mpya Real walianza kwa kasi wakifunga bao kwenye dakika ya 14 mfungaji akiwa Cristiano Ronaldo akifunga kwa mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji wa Valencia Alvaro Negredo kuunawa mpira. Bao hilo kwa Real Madrid lilidumu kwa muda mrefu kidogo na Valencia walisawazisha mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya dakika 7 kwenye dakika ya 52 mfungaji akiwa Antonio Baraggan ambaye alipiga shuti kali lililowazidi mabeki Sergio Ramos na Pepe pamoja na kipa wao Iker Casillas. Bao hilo liliamsha mashambulizi ya Valencia na haikuwachukua muda kabla ya kufunga bao la pili mfungaji akiwa beki raia wa Argentina Nicolas Otamendi ambaye alifunga kwenye dakika ya 65 ya mchezo akimaliza kwa kichwa kona iliyopigwa na Dani Parejo. Real Madrid walijaribu kusawazisha bao hilo bila mafanikio yoyote na hadi dakika 90 zinamalizika Valencia waliondoka na pointi zote 3. Huu ni mchezo wa kwanza kwa Real Madrid kupoteza rekodi yake ya kushinda michezo 22 mfululizo huku wakishindwa kuifikia na kuizidi rekodi ya timu ya Brazil ya Coritiba ambayo iliwahi kucheza mechi 24 za kiushindani bila ya kupoteza mechi hata moja. Wakati huohuo klabu ya David Moyes, Real Sociedad imefanikiwa kuizuia Barcelona kuwa vinara wa La Liga shukurani kwa goli la mapema la Jordi Alba. Ingawa kocha Luis Enrique alianza na Lionel Messi, Neymar na Dani Alves lakini walishindwa kujitetea amabapo Moyes akijihakikishia ushindi wa pili kama meneja wa Sociedad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako