• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ashuhudia mkopo ukitolewa na benki ya kwanza ya mtandao wa Internet nchini China

    (GMT+08:00) 2015-01-05 21:05:15

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang alipofanya ukaguzi mjini Shenzhen, kusini mwa China ameshuhudia mkopo wa kwanza ukitolewa na benki ya kwanza isiyoya kiserikali kwenye mtandao wa Internet.

    Akizungumzia mkopo huo wa sawa na dola za kimarekani 5600 uliotolewa kwa dereva mmoja wa lori amesema, mkopo huo mdogo ni alama ya hatua kubwa iliyopigwa kwenye mageuzi ya sekta ya fedha nchini China.

    Tofauti na benki za kawaida, benki hiyo inayojulikana kama Weizoom haina ofisi na kaunta. Aidha, mteja hapati mikopo kwa dhamana ya hati ya nyumba wala mali ya aina nyingine, isipokuwa benki hiyo itachambua uaminifu wa mteja kupitia shughuli zake kwenye mtandao wa Internet, huku teknolojia ya utambuzi wa kibaiolojia ikitumiwa wakati wa kukabidhiana mkopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako