• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • El Merrikh waituma shushushu Azam FC kujua mbinu zao

    (GMT+08:00) 2015-01-06 14:08:57
    Wapinzani wa Azam FC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huu, El Merrikh wametuma shushushu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar Tanzania ili kusoma zaidi mbinu za wapinzani wao. Azam, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), wamepangwa kuanza dhidi ya mabingwa hao mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan katika hatua ya awali ya Klabu Bingwa Afrika katikati ya mwezi ujao. Mara ya mwisho Azam na El Merrikh zilikutana katika mechi ya robo-fainali ya Kombe la Kagame iliyomalizika kwa Azam kulala kwa penalti baada ya dakika 90 kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali, Rwanda Agosti mwaka jana. Azam, inayonolewa na Mcameroon Joseph Omog, inayatumia mashindano ya Kombe la Mapinduzi kama sehemu ya maandalizi yake kabla ya kuwavaa Wasudan hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako