• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha Ebola katika hospitali ya urafiki kati ya China na Sierra leone chapanua huduma za matibabu

    (GMT+08:00) 2015-01-07 09:32:20

    Kituo cha ugonjwa wa Ebola katika hospitali ya urafiki kati ya China na Sierra leone kimeanza kutoa matibabu kwa wagonjwa watano waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola, hatua inayomaanisha kuwa kituo hicho kimepanua rasmi huduma za upimaji na matibabu.

    Hadi kufikia tarehe 5 mwezi huu, kituo hicho kilipokea watu 593 wanaoshukiwa kuambukizwa Ebola, na watu 248 kati yao wamethibitishwa kuambukziwa ugonjwa huo.

    Habari nyingine zinasema, chuo kikuu cha Oxford cha Uingereza kimeanza majaribio ya kwanza ya chanjo mpya ya Ebola, kikilenga kutoa chanjo hiyo kwa watu 72 waliojitolea kabla ya mwisho wa mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako