• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mayweather anaendeleza kufuru zake safari hii aanika utajiri wake

    (GMT+08:00) 2015-01-07 14:13:04
    Bondia Floyd Mayweather anaendeleza kufuru zake za kuanika utajiri wake kwenye ukurasa wake wa Instagram. Mayweather ambaye ni rafiki wa karibu sana wa rapper 50 Cent, amekuwa akionesha mambo mengi na haoni kama kuna ubaya kujisifia utajiri wake. Katika Instagram safari hii kaonesha vitu vingi vikiwemo magari ya kifahari, ndege na jumba. Mayweather ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa mmoja kati ya wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi kuliko wote aliingiza jumla ya dola milioni 66 kwa mwaka 2014 na moja ya vibarua alivyonavyo hivi karibuni ni pambano kati yake na Manny Pacquiao ambalo limesubiriwa kwa muda mrefu. Manny Pacquiao alipohojiwa kuhusu utajiri wa Mayweather alisema kuwa hajali kuhusu utajiri wake anachotaka ni kukutana naye ulingoni. Kama itakumbukwa kuwa mwaka jana alinyesha mvua ya dola baada ya kumwaga mapesa kwa mashabiki wake akiwa juu angani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako