Kipa wa kikosi cha kwanza cha Arsenal, Wojciech Szczesny amepigwa faini ya pauni 20,000. Szczesny amepewa adhabu hiyo baada ya kukutwa na kosa la kuvuta sigara muda mchache baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Southampton. Kitendo cha kipa huyo kilisababisha hasira kwa kocha wake Arsene Wenger na kuamua kumpa adhabu hiyo. Jack Wilshere pamoja na nahodha wa zamani wa klabu hiyo William Gallas waliwahi kukumbwa na tatizo kama hili la ufutaji wa sigara. Wakati huohuo mashabiki wengi wa soka wa Atletico Madrid wanaokadiriwa kufikia 45,000 wamempokea kwa shangwe mshambuliaji Fernando Torres Juzi Jumapili. Mashabiki wa klabu hiyo walijazana kwenye Uwanja wa Vicente Calderon kumkaribisha nyumbani mwana wao mpotevu. Torres amerudi katika klabu yake ya utotoni kwa mkopo baada ya kuwa na wakati mgumu katika klabu za Chelsea and AC Milan. Akiwa Atletico, Torres alijiwekea rekodi ya kufunga mabao 91 katika mechi 244 katika miaka yake saba kuanzia 2000 hadi 2007 alipohamia Liverpool.