Manchester United inatarajia kumtangaza kipa Mhispania, Victor Valdez kama usajili wake wa kwanza wa mwezi huu January wakati dirisha dogo la usajili likiwa wazi baada ya kipa huyo kufanya mazoezi na United kwa zaidi ya miezi miwili. Valdez alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na United ili ajiweke sawa baada ya kupona jeraha la goti ambalo limemsumbua kwa muda mrefu tangu alipokuwa na klabu ya Barcelona katikati ya msimu uliopita. Valdez alikuwa kwenye mipango ya kukamilisha uhamisho kuelekea klabu ya As Monaco kabla klabu hiyo haijafanya maamuzi mengine na kuachana naye hali iliyomfanya akose klabu baada ya kuachana na Barcelona msimu uliopita Usajili wa Valdez utaifanya United kuwa na makipa wawili raia wa Hispania baada ya kipa wake namba moja ambaye ni David De Gea ambaye hadi sasa amekuwa kwenye kiwango cha juu ndani ya klabu hiyo. Nayo klabu ya Manchester City kwa sasa ipo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Timu ya Swansea City kwa lengo la kumsajili mchezaji Wilfred Bony. Man city imepanga kutenga zaidi ya pauni milioni 30 kwa mchezaji huyo kutoka Ivory Coast mwenye umri wa mika 26, kutoka Swansea, na meneja Garry Monk amesema atahakikisha inampata Wilfred Bony katika dirisha hili la usajili.