• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sierra Leone yarefusha muda wa operesheni dhidi ya Ebola

    (GMT+08:00) 2015-01-09 10:01:09

    Sierra Leone imeamua kurefusha kwa mwezi mmoja zaidi operesheni iliyoanzishwa wiki mbili zilizopita yenye lengo la kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola. Operesheni hiyo inafanyika katika eneo la magharibi mwa Sierra Leone ikiwa ni pamoja na mji mkuu Freetown.

    Mkuu wa kituo cha kupambana na Ebola cha Sierra Leone Bw Palo Conteh amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa uamuzi huo una lengo la kuimarisha mafanikio yaliyopatikana. Pia amesema mafanikio hayo yanatokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa umma wenye ufanisi.

    Habari pia zinasema waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Bw Aminu Bashir Wali jana aliitaka jumuiya ya kimataifa kuchuka hatua za pamoja katika kupambana na Ebola. Akihutubia mkutano wa mabalozi mjini Ankara, Bw wali amesema vita dhidi ya Ebola haiwezi kupata ushindi kwa kuzitenga nchi zilizoathiriwa na Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako