Habari zinasema kwamba Chelsea imemwekea mchezaji huyo wa Barcelona kitita cha pauni millioni 200 kumnunua.
Vilevile The Blues imedaiwa kwamba iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango hicho mara mbili.
Tangu mwezi Novemba mwaka jana kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekuwa akikana habari zinazoihusisha kilabu hiyo na mchezaji Messi,lakini katika kilabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis Enrique.
Enrique hajaweza kukana madai ya kuwa na mgogoro na Messi lakini inadiwa kuwa Mesi hakushiriki katika mazoezi ya siku ya jumatatu kama alivyotakiwa.
Na kwenye habari zingine ni kwamba mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast na Swansea Wilfired Bony hadi kilabu ya Mancity unakaribia kukamilika. Ajenti wake amesema anatarajia kwamba mkataba huo utawekwa sahihi wiki hii baada ya vilabu vya Swansea na Mancity kujadiliana kuhusu kitita cha fedha kinachotarajiwa kutolewa kumnunua mchezaji huyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |