• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya gofu ya Tanzania kushiriki olimpoko mwaka ujao.

    (GMT+08:00) 2015-01-09 14:16:31
    Chama cha mchezo wa gofu nchini Tanzania (TGU) kimethibitisha kwamba kitashiriki kwenye michuano ya Olimpiki itakayofanyika huko Rio de Janeiro, Brazil ujao.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kutuma timu ya Gofu michuano ya Olimpiki tangu michuano ya mwaka 1904 ilipofanyika.

    Ushiriki wa mchezo huo, ambao utajumuisha wachezaji wanawake na wanaume katika michezo ya mmoja mmoja (individual team) kutoka katika nchi zitakazofuzu, ulipokelewa kwa shangwe na wadau wa mchezo huo kutoka nchi mbalimbali duniani, ikiwemo Tanzania.

    Makamu wa raisi wa chama hicho cha Gofu, Joseph Tango amesema wamejiandaa kwa muda mrefu na zaidi ya vijana 60 kutoka vilabu mbalimbali nchini wanaandaliwa ili kupata timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya kufuzu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako