KLABU ya KCB, inakabiliwa na mtihani mkali wa iwapo itamrejesha tena straika wao wa zamani Paul Mungai Kiongera anayeuguza jeraha kwa sasa na ambaye anaichezea miamba Simba SC wa Tanzania.
Bado KCB haijaamua iwapo itakuwa sahihi kumchukua Kiongera kwa mkopo wa miezi sita katika kipindi hiki ambacho anaendelea kupata nafuu kutokana na upasuaji wa jeraha la goti alilofanyiwa India mwaka uliopita.
Hata hivyo Meneja wa KCB, Joseph Okal amesema wamekuwa wakilijadili swala hilo na Simba na wamekubali kutoa Kiongera kwa KCB kwa njia ya mkopo kwa kipindi cha miezi sita ijayo.
Paul Kiongera kwa upande wake amesema ana matumaini ya kwamba kufikia mwezi ujao Februari atakuwa amepona na tarayi kabisa kurejea ulingoni kufanya makamuzi yake.
Kiongera alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea KCB kwa dau la zaidi ya shilingi milioni moja na baada ya kushiriki mechi tatu na kupachika magoli mawili, akapata jeraha jeraha la goti ambalo limekuwa likimtatiza tangu alipokuwa Gor Mahia.
Jeraha hilo lilimweka nje kwa miezi miwili kabla ya klabu yake kuamua kugharamia matibabu ya upasuaji wake kule India.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |