Mchezaji wa Wolfsburg Junior Malanda afariki dunia kwenye ajali ya gari
(GMT+08:00) 2015-01-12 14:01:56
Mchezaji wa kiungo katika kilabu ya Wolfsburg nchini Ujerumani Junior Malanda ambaye pia anachezea timu ya vijana ya kimataifa ya Ubelgiji amefariki dunia katika ajali ya barabarani. Ajali hiyo ilitokea Jumamosi karibu na Bielefeld magharibi mwa Ujerumani wakati Malaba alipokuwa safarini kukutana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kushiriki kwenye kambi ya mazoezi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliripotiwa kukaa katika kiti cha nyuma ya gari ambapo kulingana na maafisa wa polisi wa Ujerumani lilikuwa likipelekwa kwa mwendo wa kasi hata hivyo dereva na abiria mwingine wote wakiwa ni Wabelgiji wenye miaka 20 walijeruhiwa vibaya. Malanda alitarajiwa kuondoka na kwenda Afrika kusini na wenzake kwenye kambi ya Wolfsburg juzi jumamosi, lakini klabu iliahirisha kuondoka na ilikuwa jana iamualiwe kama watakwenda au la.