• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona kufanya uchaguzi wa rais, Suarez, Messi na Neymar waifurahisha timu

    (GMT+08:00) 2015-01-12 14:02:59
    Katika muendelezo wa kizaazaa kinachoikabili Barcelona, Rais Jose Maria Bartomeu ametangaza kuwa klabu hiyo itafanya uchaguzi wake mwaka huu akirudisha nyuma uchaguzi huo ambao awali ulipangwa kufanyika mwaka 2016. Hii ni kutokana na shinikizo kubwa ambalo amepata toka kwa wanachama wa klabu hiyo ambao wanafahamu kiini cha migogoro inayoendelea sasa kuwa ni uongozi mbovu uliokuwepo kwenye klabu hiyo chini ya rais wa awali Sandro Rosell ambaye alijiuzulu mwaka jana. Moja kati ya majina mabayo yamekuwa yakitajwa kuhusika na uongozi mpya ni rais wa zamani Joan Laporta ambaye amekuwa akisema wazi kuwa anataka kurudi kuiongoza klabu hiyo. Wakati huohuo timu hiyo jana ilicheza ambapo Luis Suarez alitoka kimasomaso na kufanikiwa kufunga kwenye ligi ya La Liga walipocheza dhidi ya Atletico Madrid na kidogo kupunguza shinikizo kwa kocha wao Luis Enrique. Wengine walioingiza magoli kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa Barcelona kuondoka vifua mbele kwa magoli 3-1ni Lionel Messi na Neymar.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako