• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ebola yaweka hatarini maendeleo ya Liberia na Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2015-01-13 10:15:39
    Ripoti mbili zilizotolewa Jumatatu na Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa, athari ya maambukizi ya Ebola kwa jamii na uchumi nchini Liberia na Sierra Leone itaendelea kwa muda mrefu, na kuyaweka hatarini maendeleo ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.

    Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amenukuu ripoti hizo akisema, ajira zinazopotea ni nyingi kuliko zinazorudishwa, karibu nusu ya kaya za Liberia zimepoteza ajira. Amesema nchini Sierra Leone mapato ya wafanyakazi wasio wakulima wanaojiajiri yanapungua sana katika maeneo ya mijini.

    Ripoti hizo zimetolewa kwa mujibu wa takwimu zinazotokana na uchunguzi wa simu za mkononi, ambao ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Benki ya Dunia za kukabiliana maambukizi ya Ebola.

    Habari nyingine zinasema kitengo cha Ebola kilichofadhiliwa na China nchini Liberia kimewaruhusu wagonjwa watatu wa Ebola kuondoka kwenye kituo hicho baada ya vipimo vilivyofanywa mara mbili kuonyesha kuwa hawana virusi vya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako