Pambano kati ya Pacquiao na Mayweather kuanikwa wazi mwezi
(GMT+08:00) 2015-01-14 14:06:22
Bondia Manny Pacquiao kwa uhakika mkubwa amesema mwisho wa mwezi huu itawekwa wazi kuhusu pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather. Pambano hilo litakalomaliza ubishi wa nani bondia mkali kati ya wawili hao linatajwa kuwa na thamani ya Dola milioni 300 na litafanyika kwenye Ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas, Mei 2 mwaka huu. Pacquiao mara kwa mara amekuwa akimtaka Mayweather ulingoni hasa baada ya kumchapa Chris Algieri, Novemba mwaka jana na sasa amesema pambano dhidi ya Mayweather litatangazwa kabla ya Februari. Mayweather anataka pambano likifanyika iwe Mei 2, lakini tatizo ni kwamba siku hiyo Miguel Cotto anatarajia kuzichapa na Saul 'Canelo' Alvarez kwenye pambano lenye uhasama mkubwa. Mayweather alisema mwezi uliopita kuwa watu wanataka pambano hili na wao mabondia wote wawili wanataka ila inaonekana kuna tatizo kwa promota wa Pacquiao Bob Arum.