Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameonesha kutokuwa na uhakika wa kubakia katika klabu yake baada ya kukiri kuwa hajui atakuwa kwenye klabu gani mwakani. Nahodha huyo wa Argentina wikiendi iliyopita alikanusha uvumi unaomuhusisha yeye kuwa ana mpango wa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu za Chelsea na Manchester City zinazomuwania na kusisitiza kuwa hizo ni redio vifua tu. Lakini juzi Jumatatu kwenye sherehe ya utoaji wa tuzo za mchezaji bora wa dunia Ballon d'O alikiri kwamba hajajua hatma itakuwaje. Katika tuzo hizo alishindwa na mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kama mchezaji bora wa dunia. Taarifa za kutoelewana na kocha wake Luis Enrique ndio inaonekana chanzo cha Messi kutaka kuondoka katika klabu hiyo iliyomkuza. Mkataba wa sasa wa Messi unatarajia kufika kikomo mwaka 2019.