• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha tatu cha madaktari wanajeshi wa China chaelekea Sierra Leone kusaidia kupambana na Ebola

    (GMT+08:00) 2015-01-14 20:13:54

    Kikosi cha tatu cha madaktari wanajeshi wa China kimeondoka Beijing na kuelekea Sierra Leone kwa ajili ya kubadilishana zamu na kikosi cha pili na kuendelea kutekeleza majukumu ya kupambana na maambukizi ya Ebola katika miezi miwili ijayo.

    Kwa mujibu wa makubaliano kati ya China na Sierra Leone, licha ya kusaidia kupambana na Ebola, kikosi hicho pia kitatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa mashirika ya matibabu nchini humo.

    Imefahamika kuwa ikilinganishwa na vikosi viwili vilivyopita, idadi ya madaktari wataalamu na wauguzi wakuu imeongezeka kwenye kikosi cha tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako