• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Equatorial Guinea awanunulia mashabiki tiketi

    (GMT+08:00) 2015-01-15 14:05:13
    Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema, amelipia tiketi elfu 40 ili kuhakikisha mashabiki wanahudhuria kombe la Mataifa ya Afrika. Nchi hiyo imechukua nafasi ya Morocco kuwa mwenyeji mwezi uliopita tu na kuna wasiwasi kuwa michezo hiyo haitahudhuriwa na watu wengi. Rais huyo amesema lazima wanunue tiketi ili kujaza uwanja na kuwashawishi wale wenye uwezo kuwasaidia wasionao huku akijitolea mfano yeye mwenyewe kwa kununua idadi hiyo ya tiketi na kukadiria kuwa kila mkoa utakuwa na tiketi elfu 10. Mikoa anayoitaja hapa ni minne inayoandaa michuano hiyo ambayo ni Malabo, Bata, Ebebiyin na Mongomo. Nguema ameongeza kuwa bei ya kununulia tiketi itakuwa ni FCFA 500 sawa na euro 0.7. Na ili kuwahamasisha zaidi watu kwenda viwanjani kuangalia michuano hiyo inayoanzia Jumamosi hii tarehe 17 hadi Februari 8, saa za kazi zimepunguzwa kwa saa mbili katika siku za mechi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako