Huku Abdoulshakur Kabura wa burundi akipata ushindi kwa seti 4-6 6-4 6-4 dhidi ya Damien Laporte wa Sychelles. Katika michezo mingine Ernest Habiyambere wa Rwanda amemchapa Emanueli Malya wa Tanzania kwa jumla ya seti 4-6 7-6 na 6-4. Yabsira Kadebe wa Ethiopia ameibuka kidedea kwa kumchapa Radjabu Ntambi wa Burundi kwa 6-2 6-2. Kwa upande wa fainali ya wawili wawili Abdoulshakur Kabura na Jonathan Mugisha wa burundi wamewachapa Ryan Randiek na Keen Shan wa Kenya kwa seti 6-1 6-2. Abraham Adelin na Georgina Kemmy wa Tanzania wamepata ushindi wa seti 6-1 6-1 dhidi ya Mwamini Bitungwa na Mariam Mujawiana wa Burundi. Washindi watano wa jumla toka katika kila kundi wataenda kushiriki michuano ya tenesi ya Afrika kwa vijana itayofanyika Nchini Tunisia mwezi Machi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |