• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kupokea ujumbe mzito wa Arsenal wikiendi hii

    (GMT+08:00) 2015-01-16 14:05:24
    Klabu ya Arsenal imepanga kutuma maofisa wake wa biashara jijini Dar es Salaam tanzaniza kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano na wafanyabiashara kadhaa wakubwa. Huu utakuwa ujumbe wa kwanza kabisa wa Arsenal nchini Tanzania ambapo klabu hii kubwa ya Ligi Kuu England inataka kujenga ushirika katika maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua mafanikio yaliyofikiwa kwenye nchi nyingine za Afrika zikiwamo Kenya, Uganda na Nigeria. Ofisa Biashara Mkuu wa Arsenal, Venkatesham alisema wameichagua Tanzania kwani wana mashabiki wengi na kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania, watakuwa karibu zaidi na mashabiki wao kuliko ilivyokuwa awali. Wajumbe hao wa jopo la Maendeleo ya Ushirikiano ya Arsenal wanatarajiwa kuwasili Tanzania Januari 18 na kukaa kwa wiki moja jijini Dar es Salaam, wakiitisha mikutano kadhaa na wafanyabiashara.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako