• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pambano kati ya Pacquiao na Mayweather makubaliano bado hayafikiwa

    (GMT+08:00) 2015-01-16 14:06:47
    Pambano la masumbwi linalosubiriwa na ulimwengu mzima kati ya mabondia wawili bora katika miaka ya hivi karibuni Floyd Mayweather na Manny Pacquiao linakaribia kutokea baada ya uthibitisho wa mazungumzo ya pande mbili zinazowakilisha mabondia hao. Wakala wa Bondia Mfilipino Pacquiao, Fred Sternburg amethibitisha kuwa mazungumzo baina ya kambi za mabondia hawa wawili yanaendelea vizuri na huenda makubaliano yakafikiwa siku sio nyingi. Wakala huyo hata hivyo amekanusha kuwepo kwa uthibitisho wa tarehe ya mabondia hao kupanda ulingoni baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa wawili hao watapambana Mei mbili mwaka huu. Pambano hili limewahi kuandaliwa kwa muda mrefu bila mafanikio baada ya mabondia hawa kuonekana wakikwepana hususan Floyd ambaye alikuwa akitoa visingizio vya kila aina ikiwemo kutaka mpinzani wake apimwe vipimo vya dawa za kulevya. Taarifa zaidi zinasema kuwa mabondia hawa wamekubaliana kugawana asilimia 60 kwa 40 ya mapato ya pambano hili ambapo Floyd atachukua asilimia 60 na Manny atachukua asilimia 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako