• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za FBI kufanyika Tanzania Usain Bolt kushiriki

    (GMT+08:00) 2015-01-19 14:08:19
    Mwanariadha nyota na bingwa wa dunia wa mita 100, Usain Bolt kutoka Jamaica amealikwa kushiriki mbio za kimataifa za FBI zitakazofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Mbio hizo zimeandaliwa na mwandaaji wa kimataifa, Al Franken na mwanawe Don zikilenga kumuenzi mwanariadha wa zamani, Filbert Bayi ambaye aliweka rekodi kwenye mbio za maili moja ambazo zimeitwa Miracle Mile. Tayari, maandalizi ya mbio hizo yameanza na zitafanyika kwa usimamizi wa Shirikisho la Riadha la Dunia (IAAF), Riadha Tanzania (RT), klabu ya michezo ya Hanang na Taasisi ya Filbert Bayi (FBF). Katibu Mkuu wa klabu ya Hanang Wilhelm Gidabuday alisema lengo la mbio hizo ni kuwaenzi wanariadha waliowahi kuiletea sifa nchi na kusisitiza kuwa tayari amemaliza tofauti yake na Bayi na Suleiman Nyambui kwa manufaa ya Taifa. Mbio za FBI zitakuwa za viwanjani kuanzia mbio za mita 100 hadi 10,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako