• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mali yatangaza kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola

    (GMT+08:00) 2015-01-19 19:59:28

    Serikali ya Mali imetangaza kuwa maambukizi ya Ebola yamemalizika nchini humo kwa kuwa hakuna kesi yoyote mpya ya ugonjwa huo iliyoripotiwa ndani ya siku 42 zilizopita.

    Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, waziri wa afya wa Mali Osman Kone amesema tarehe 6 Decemba mwaka jana mgonjwa wa mwisho aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini Mali alipona na kuondoka hospitali.

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini Mali Ibrahima Soce Fall amesema, kutokana na kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani WHO, kama hakuna maambukizi mapya ndani ya siku 42, nchi husika inaweza kutangaza kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

    Wakati huohuo, nchi nyingine tatu za Afrika Magharibi Guinea, Liberia na Sierra Leone zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo zimeshuhudia kupungua kwa maambukizi mapya. Serikali ya Liberia imekadiria kuwa haitakuwa na kesi mpya hadi kufikia mwishoni mwa Februari, huku Sierra Leone ikisema itafikia lengo hilo mwishoni mwa Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako