• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sierra Leone yaanzisha kampeni ya kutokomeza Ebola

    (GMT+08:00) 2015-01-20 10:10:51

    Sierra Leone imeanzisha kampeni mpya ya kutokomeza ugonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Freetown na vitongoji vyake. Mkurugenzi mkuu wa kituo cha taifa cha kupambana na Ebola Bw Panto Conteh amesema awamu hiyo ya pili inalenga kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo na kuimarisha mafanikio ya awamu ya kwanza iliyofanyika kati ya Disemba 17 2014 na Januari 15 2015.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Bw Conteh amesema kwa ujumla hali katika eneo la magharibi imeimarika, lakini kuna baadhi ya maeneo yanayotakiwa kusafishwa kabisa, kukaguliwa na kupangwa upya. Amesema katika awamu ya kwanza, jumla ya wagonjwa 9,334 walikimbizwa hospitali ambapo 263 kati yao waligunduliwa kuwa na virusi vya Ebola na hatimaye kupelekwa katika vituo maalum kwa matibabu ya Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako