• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasiwasi wazuka kwa mashabiki baada ya Yaya Toure kukosa mazoezi

    (GMT+08:00) 2015-01-20 15:32:57
    Kiungo wa Ivory Coast, Yaya Toure juzi Jumamosi hakufanya mazoezi na wenzake wakati kikosi hicho kilipokuwa kikijiandaa na mechi yake ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2015) itakayopigwa leo. Kitendo hicho kilizua hofu kwa mashabiki kwamba huenda ni majeruhi jambo ambalo litakuwa pengo kubwa katika kikosi hicho cha Afrika Magharibi. Mwanasoka huyo bora wa Afrika mara nne alikuwa nje ya uwanja wakati wachezaji wenzake walipokuwa wakiendelea na mazoezi katika uwanja mdogo uliopo mjini Malabo. Ivory Coast imepangwa kwenye Kundi D na mechi yake ya kwanza itacheza dhidi ya Guinea mjini Malaboleo, huku mchezo mwingine katika kundi hilo ukitarajia kuzikutanisha Mali na Cameroon. Yaya Toure ni nyota muhimu katika kikosi hicho cha Ivory Coast katika mipango yake ya kubeba ubingwa wa Afcon 2015 baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa miaka mingi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako