• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GDP ya China yaongezeka kwa asilimia 7.4 kwa mwaka 2014

    (GMT+08:00) 2015-01-20 20:06:24

    Takwimu zilizotolewa leo na mamlaka ya takwimu ya China zimeonesha kuwa thamani ya jumla ya uzalishaji GDP ya China iliongezeka kwa asilimia 7.4 kwa mwaka 2014 na kufikia dola za kimarekani trilioni 10.4. Kasi hiyo ya ukuaji wa GDP ni ndogo zaidi katika miaka 24 iliyopita, hata hivyo inalingana na matarajio ya soko, wakati Chinanchi hiyo ikinakumbatia hali mpya ya kawaida ya uchumi wake ambao unasisitiza kupunguza kasi ya ongezeko lakini kuongeza ubora wake.

    Akizungumzia ongezeko hilo, Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Ma Jiantang akizungumzia ongezeko hilo anasema, ukuaji wa uchumi wa China mwaka jana uko katika viwango vinavyokubalika, na kutimiza lengo la ongezeko la asilimia 7.5.

    "Uchumi wetu uliongezeka kwa asilimia 7.4, lakini tukiangalia nafasi za ajira, nafasi zaidi ya milioni 13 zimebuniwa, kiwango cha kutokuwa na kazi ni asilimia 5.1 na faharisi ya matumizi ya walaji CPI iliongezeka kwa 2%, na tukiweka takwimu hizo nne kwa pamoja, tuaweza kusema ukuaji wa uchumi uko katika viwango viunavyoeleweka."

    Ma amesema takwimu hizo pia zinaonesha kuwa uchumi wa China unaelekea kwenye kiwango cha kati na kiwango cha juu.

    "Sekta ya teknolojia ya juu iliongezeka kwa ailimia 12.3, na kuchukua asilimia zaidi ya 10 ya sekta nzima ya viwanda. Aidha, biashara kupitia mtandao wa Internet imeongezeka kwa kasi, ambapo mauzo ya rejareja kwenye internet yameongezeka kwa asilimia 49.7."

    Akizungumzia maendeleo ya uchumi wa China kwa mwaka huu, Ma amesema ongezeko la kasi litadumishwa, ingawa uchumi wa China unakabiliwa na changamoto na utata mwingi ndanichini na nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako